Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia ya nyuklia yarejesha kicheko kwa wanafunzi Zimbabwe

Teknolojia ya nyuklia yarejesha kicheko kwa wanafunzi Zimbabwe

Pakua

Mabadiliko ya tabianchi yameendelea kuwa mwiba si tu kwa wavuvi bali pia wakulima ambao ukame sasa umesababisha washindwe kupata mazao ya kutosha ili waweze kuuza kwa ajili ya kipato na pia kwa ajili ya mlo. Mathalani nchini Zimbabwe ambako ukame wa miaka mitatu mfululizo ulileta zahma kubwa, wakulima wakawa hawana la kufanya na watoto nao wakashindwa kwenda shule. Hata hivyo teknolojia ya sayansi ya nyuklia kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA pamoja na utaalamu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO, imeleta nuru si tu kwa wakulima bali pia watoto wao, ni kwa vipi basi? Grace Kaneiya anafafanua kwenye makala hii.

Audio Credit
Assumpta Massoi/Grace Kaneiya
Audio Duration
4'4"
Photo Credit
IAEA Video