Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tukishikamana tutaweza kulinda mazingira Uganda:Wanahabari

Tukishikamana tutaweza kulinda mazingira Uganda:Wanahabari

Pakua

Changamoto za ulinzi wa mazingira ni mtihani unaozikabili nchi nyingi hasa kutokana na umasikini unaochangia wengi kuingia katika shughuli za uharibifu wa mazingira. Umoja wa Mataifa unaendelea kuzihimiza nchi wanachama kuchukua hatua ili kukabiliana na athari za uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuacha ukataji miti hovyo kwa ajili ya uchomaji mkaa, kuharibiwa kwa vyanzo vya maji na uharibifu mwingine. Nchini Uganda sasa wanahabari wameamua kulishikia bango suala la kuchagiza jamii kuhifadhi mazingira ikiwemo upanzi wa miti. Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego amehudhuria uzinduzi wa kampeni hiyo ya wanahabari ya upandaji miti kulinda mazingira na kutuandilia makala hii.

 

Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kibego
Audio Duration
3'44"
Photo Credit
UN Photo/Isaac Billy