Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasio na utaifa wapata msaada kutoka kwa chama cha wanawake cha misaada ya kisheria Côte d’Ivoire

Wasio na utaifa wapata msaada kutoka kwa chama cha wanawake cha misaada ya kisheria Côte d’Ivoire

Kutokuwa na utaifa ni moja ya changamoto kubwa inayowakabili sio tu wahamiaji, bali pia wakimbizi, waomba hifadhi, watu waliotawanywa na majanga na hata waliozaliwa katika nchi ambazo sheria haziwaruhusu kuwa na utaifa kama wazazi wao si raia. Kufuatia wito wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana na changamoto hii katika kila nchi na kuhusisha wadau wote zikiwemo asasi za kiraia hatua zimeanza, mathalani nchini Côte d’Ivoire  ambako wataalamu wa misaada ya kisheria kutoka Chama cha misaada ya kisheria cha wanawake wanafanya kampeni dhidi ya tatizo la kukosa utaifa Kijiji hadi Kijiji ili kuwaelimisha watu jinsi ya kupata nyaraka za kisheria zinazoeleza haki zao. 

Photo Credit
UNHCR