Changamoto kubwa katika kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu, ni uelewa-Winnie Mtevu

Changamoto kubwa katika kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu, ni uelewa-Winnie Mtevu

Pakua

Tatizo la usafirishaji na biashara haramu ya binadamu linaongezeka kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa zilizotolewa mwanzoni mwa mwaka huu wa 2019 kote duniani. Pia takwimu zilizotolewa na shirika la kazi duniani ILO mwishoni mwa mwaka jana 2018 zinasema watu takribani milioni 40 kote duniani bado ni waathirika wa utumwa au kutumikishwa kinyume cha matakwa yao.

Winnie Mtevu kutoka asasi ya Haart Kenya inayojishughulisha na uzuiaji wa biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu katika mahojiano na Patrick Newman kandoni mwa jukwaa la baraza la kiuchumi na kijamii la umoja wa Mataifa ECOSOC, lililofanyika mwaka huu jijini NewYork Marekani anasema moja ya changamoto kubwa katika vita hivi ni watu wengi kutofahamu kuhusu unyama huu.

Audio Credit
Patrick Newman/Winnie Mtevu
Audio Duration
2'28"
Photo Credit
Picha na UN/ Loey Felipe