Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukinyamaza utalizwa, sema usikike:Mradi wa Tanzania Bora

Ukinyamaza utalizwa, sema usikike:Mradi wa Tanzania Bora

Pakua

Tatizo la ukatili wa kijinsia hususan dhidi ya wasichana na wanawake ni jinamizi linaloighubika dunia na Umoja wa Mataifa na wadau wake wanalishikia bango wakihimiza serikali, asasi za kiraia na kila mtu kuchukua hatua kulikomesha. Mbinu mbalimbali ikiwemo mikutano na elimu vimetumika lakini bado halijaisha. Sasa vijana wameamua kutafuta mbinu za kibunifu ili kusaidia katika kampeni hizo. Moja ya vijana waliochukua hatua ni Abella Bateyunga mjasiriamali na mbunifu kutoka mradi wa Tanzania Bora. Yeyé na wenzake wamebuni “kanga data fashion”.

Kanga ni vazi mashuhuri kwa wanawake na wasichana nchini Tanzania lakini kanga hii si ya kuvaliwa kwa maonyesho  tu bali ni ya kuelimisha na kufikisha ujumbe. Haya inafikishaje ujumbe huo uangana naye akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii na kwanza anafafanua kuhusu ubunifu huo.

Audio Credit
Arnold Kayanda/Flora Nducha/Abella Bateyunga
Audio Duration
5'23"
Photo Credit
K15 Photos