Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajira si lazima uipate ofisini unaweza kujiajiri :Mpishi Smart

Ajira si lazima uipate ofisini unaweza kujiajiri :Mpishi Smart

Pakua

Changamoto za ajira kwa vijana ni kilio cha kila kona duniani. Kwa mujibu wa takiwmu za shirika la kazi duniani ILO idadi ya vijana wasio na ajira hivi sasa ni zaidi ya milioni 70 na inaendelea kuongezeka huku Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara zaidi ya vijana milioni 12 wanaopaswa kuwa katika soko la ajira hawana kazi.

Kwa kutambua changamoto hiyo vijana mbalimbali wameamua kuchukua hatua ili kubadili mwenendo huo kwao binafsi, kwa vinaja wenzao na jamii zao . Na hatua hiyo ni kuja na ubunifu ambao sio tu utawapa kitu cha kufanya bali pia utawapa kipato na kubadili fikra za kwamba ajira ni lazima ukae ofisini au kuajiriwa na mtu, bali unaweza kujiajiri. Miongoni mwa vijana hao ni Frank Salila mkurugenzi na muasisi wa taasisi ya Mpishi Smart ambayo pamoja na miradi mingine imeanzisha App ya kuwasaidia wajasiriamali wa chakula kuwafikia wateja wao.

Katika makala hii Frank anazungumza na Stella Vuzo wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es Salaam kuhusu taasisi yake na wanachokifanya.

Audio Duration
5'4"
Photo Credit
UNEP Asia Pacific