Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana Tanzania msisalie watazamaji wa harakati za maendeleo, jumuikeni- Mulika

Vijana Tanzania msisalie watazamaji wa harakati za maendeleo, jumuikeni- Mulika

Pakua

Umoja wa Mataifa kupitia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs au ajenda 2030 unataka serikali, mashirika na asasi mbalimbali kuhimza jamii ulimwenuni hususan vijana  kushiriki kikamilifu katika miradi mbalimbali  ya kimaendeleo ili kuweza kufikia malengo hayo ifikapo mwaka 2030.

Vijana ambao ndio wameshika usukani wa mustakabali wa dunia wanachagizwa kusaka na kutumia fursa za kimaendeleo ili kuweza kujikwamua na changamoto zinazowakabili ikiwemora ajira.

Na je wanafanya nini? Au je wameitikia wito huo? Katika makala hii Flora Nducha wa Idhaa ya kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Hussein Melele, Mkurugenzi wa Mulika Tanzania, ambayo ni asasi ya kiraia yenye  lengo la kuwahimiza vijana kushiriki katika miradi  mbalimbali yenye fursa ili waweze kujikwamua kiuchumi, kisiasa na kijamii badala kubakia kuwa wapokeaji tu wa miradi. Bwana Hussein anaanza kwa kuelezea jinsi vijana wanavyoshirikishwa katika miradi  mbalimbali ya kimaendeleo kupitia asasi yake.

Audio Credit
Arnold Kayanda/Flora Nducha
Audio Duration
4'2"
Photo Credit
UN SDGs