Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baadhi ya watu wanaozaliwa na hali ya kutoweza kujifunza Uganda hukosa haki zao

Baadhi ya watu wanaozaliwa na hali ya kutoweza kujifunza Uganda hukosa haki zao

Pakua

Katika mfululizo wa uchambuzi wa ibara za Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa leo tunaangazia ibara ya 2. Ibara hii inasema kwamba 

“Kila mtu anastahili kuwa na haki zote na uhuru wote ambao umeelezwa katika tamko hili bila ubaguzi wa aina yoyote kama vile rangi, taifa,jinsia, lugha,,dini,siasa,fikra,asili ya taifa la mtu,miliki, kuzaliwa au kwa hali nyingine yoyote.

Hali kadhalika hakuna ubaguzi utakaotendwa kwa misingi ya kisiasa, kimamlaka au hadhi ya kimataifa ya nchi au utawala ambao mtu fulani anatoka,iwe ni huru,iwe chini ya udhamini,isiyojitawala au chini ya  mazingira mengine yenye udhibiti wa kimamlaka.” Licha ya serikali kutia saini na kuridhia tamko hili bado baadhi ya wananchi wanakumbwa na sintofahamu na kunyimwa haki zao za msingi kwa mujibu wa ibara hii.

Miongoni kwa haki hizo ni ile ya kupatiwa huduma bila kujali hali yoyote ambayo mtu amezaliwa nayo. Mfano kwa baadhi ya watu waliozaliwa na hali ya kutokuwa na uwezo wa kujifunza, au Down Syndrome huduma za msingi kama vile afya na elimu zinakuwa ni tabu, mathalani nchini Uganda ambako Siraj Kalyango katika makala hii amefuatilia kuweza kuona hali ikoje kwa kuzingatia ibara hii ya 2 ya Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.

 

Audio Credit
Anold Kayanda/Siraj Kalyango
Audio Duration
4'9"
Photo Credit
World Bank/Dominic Chavez