Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umaskini bado ni changamoto kwa baadhi ya wananchi wa Burundi

Umaskini bado ni changamoto kwa baadhi ya wananchi wa Burundi

Pakua

Leo ikiwa ni siku ya kutokomeza umaskini duniani, ambalo ni lengo la kwanza la malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs Umoja wa Mataifa unasema bado watu milioni 700 kote ulimwenguni wanaishi kwenye lindi la umaskini, bila kufahamu mlo wao wa kesho utatoka wapi, bila kuwa na uhakika pia wa kipato cha kuwezesha familia kukimu mahitaji mengine muhimu ya kila siku.

Miongoni mwa watu hao milioni 700 wako nchini Burundi ambako licha ya jitihada za serikali, hali ya baadhi ya wananchi ni tabu. Je ni umaskini huo ni kwa kiasi gani? Ramadhani Kibuga mwandishi wetu wa Maziwa Makuu amevinjari mjii Mkuu wa Burundi, Bujumbura na kutuandalia ripoti ifuatayo.

 

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/Ramadhani Kibuga
Audio Duration
4'1"
Photo Credit
Watoto nchini Burundi wanaopokea mlo shuleni.(Picha:WFP/Didier Bukuru)