Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nilimeza zaidi ya vidonge 80 ili nijiue-Sheila

Nilimeza zaidi ya vidonge 80 ili nijiue-Sheila

Pakua

Takriban watu laki nane hufariki dunia kila mwaka kutokana na kujiua. Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya shirika la afya ulimwenguni WHO, kujiua ni sababu kuu ya pili miongoni mwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 29 kote ulimwenguni.

Kujiua ni janga la dunia huku asilimia 79 ya vifo vilivyotokana na kujiua mwaka 2016 vikitokea katika nchi zenye kipato cha chini na cha wastani.

WHO inasema kwa kila mtu mzima anayejiua kuna zaidi ya watu 20 waliojaribu kujiua. Katika kusaka sababu na hata visa vinavyochochea hali hiyo, Grace Kaneiya wa idhaa hii amezungumza na Sheila Akwara kutoka Kenya ambaye amehamia Marekani. Sheila alitaka kujiua zaidi ya mara moja lakini akanusurika. Je nini kilichochoea? Ungana nao basi katika makala hii awamu ya kwanza ambapo Sheila anaanza kwa kuelezea maisha yake ya utotoni

Soundcloud
Audio Credit
Siraj Kalyango
Audio Duration
4'27"
Photo Credit
UNICEF/Adriana Zehbrauskas