Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makazi mapya yanayozingatia mazingira yaleta ahueni kwa wakimbizi wa Yemen

Makazi mapya yanayozingatia mazingira yaleta ahueni kwa wakimbizi wa Yemen

Pakua

Yemen, nchi iliyogubikwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe zaidi ya miaka mitatu sasa. Mamia ya maelfu ya raia wamefurushwa makwao na sasa wanaishi ndani au nje ya nchi hiyo. Maisha ya ukimbizini ni magumu na yanakuwa magumu zaidi pale ambapo makazi ambayo unaishi hayahimili joto wala baridi. Jua linakuwa lako, halikadhalika mvua. Hali hiyo ndio imekumba wakimbizi wa Yemen waliosaka hifadhi kwenye moja ya majimbo  ya nchi hiyo. Hata hivyo sasa nuru imewageukia kwa kuwa Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la kuhudumia wakimbizi, UNHCR umechukua hatua kuhakikisha hata kama ni wakimbizi, wanaishi kwenye makazi bora na si bora makazi. Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi anakupasha kwa kina kupitia makala hii.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
3'49"
Photo Credit
Giles Clarke for UNOCHA