Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilimo hai na nuru huko Gabon

Kilimo hai na nuru huko Gabon

Pakua

Uhifadhi wa mazingira unakwenda sambamba na kilimo bora kinachohakikisha kuwa wakulima hawakwatui hovyo ardhi na hivyo kusababisha mmomonyoko wa udongo. Kama hiyo haitoshi, wakulima huelekezwa jinsi ya upanzi bora wa mbegu kuhakikisha kuwa wanapopalilia, basi wanahifadhi pia udongo. Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO limechukua hatua hiyo huko Gabon ambako jiwe moja limeua ndege watatu. Kilimo hai kimewezesha kuanzishwa kwa ushirika, wakulima wanalima eneo kubwa zaidi kwa muda mfupi, bila kusahau uhifadhi wa mazingira na mazao kama njia ya kuepusha njaa, lengo la pili la malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Je nini kimefanyika? Siraj Kalyango anakupasha zaidi.

Audio Credit
Siraj Kalyango
Audio Duration
4'
Photo Credit
UN