Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa serikali walenga kukabiliana na umaskini Uganda

Mpango wa serikali walenga kukabiliana na umaskini Uganda

Pakua

Licha ya kwamba umaskini katika dunia umetokomezwa kwa nusu tangu 2000, juhudi madhubuti zinahitajika ili kuimarisha mapato ya watu, kuondoa mateso na kujenga mbinu za kustahimili umaskini uliokithiri hususan katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara. 

Ili kufanikisha lengo hili la kwanza la malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa nchi mabli mbali zimeweka mikakati ili kufanikisha hili. Nchini Uganda serikali imechukua hatua na kuanzisha mradi wa kutokomeza umaskini kupitia kilimo basi ungana na John Kibego katika Makala akizungumza na Luteni  Kahwa wa jeshi la Uganda la UPDF.  

Audio Credit
John Kibego
Audio Duration
3'31"
Photo Credit
Stephan Gladieu/World Bank