Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zeze na gitaa mikononi mwa vijana kutoka vitongoji duni Brazil

Zeze na gitaa mikononi mwa vijana kutoka vitongoji duni Brazil

Pakua

Juma hili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa  kundi la vijana kwa jina Camerata kutoka vitongoji duni vya mji wa Rio de Janeiro nchini Brazil wamezuru Umoja huo. 

Vijana hawa walicheza aina ya muziki wa dhati au Classical uliotungwa na Mozart na Bach na pia watungaji kutoka Brazil. Licha ya mazingira walimokulia wamejifunza kucheza zeze ambalo kwa kawaida huchukuliwa kama ala ya kifahari. 

Kundi hili la Camerata linafadhiliwa na shirika la kiraia lenye lengo la kuimarisha elimu ya masuala ya  kitamaduni na ujumuishwaji katika jamii kwa kufundisha muziki wa dhati. Kupitia njia hii vijana wanajiepusha na matendo maovu na kujikuta kwa njia moja au nyingine wanashiriki katika kuleta amani kama anavyosimulia Grace Kaneiya aliyefuatilia tumbuizo hilo.

Audio Credit
Siraj Kalyango, Grace Kaneiya
Audio Duration
52"
Photo Credit
UN News