Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulaya na Asia ya Kati zaingia katika mfumo mpya wa utapia mlo:FAO

Ulaya na Asia ya Kati zaingia katika mfumo mpya wa utapia mlo:FAO

Pakua

Ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo FAO inasema Ulaya na Asia ya Kati inaingia katika mfumo mpya wa utapiamlo, ikiainisha ongezeko la utipwatipwa na maradhi mengine yanayoambatana na hali hiyo.

Shirika hilo linasema ukuaji wa uchumi na kuongezeka kwa kipato vimesaidia kuondoa njaa katika kanda hizo lakini pia umesababisha mabadiliko ya mfumo kwa walaji na kusababisha tishio na adha zingine za kiafya.

Ripoti hiyo “Mtazamo wa kikanda wa uhakika wa chakula :Ulaya na Asia ya Kati” inatathimini takwimu za utajiri wa nchi katika usambazaji wa lishe, viashiria vya lishe dunia kama vile matatizo ya kudumaa, kupoteza uzito, anemia, uzito wa kupindukia, na utipwatipwa, lakini pia watu kwa wastani wanakula nini.

Ripoti hiyo inaonyesha mabadiliko kutoka nchi kukabiliana na lishe duni na ukosefu wa vitamin na kuingia katika kupambana na maradhi yanayosababishwa na ongezeko la vyakula vya mafuta, sukari, nyama, mazima na vyakula vya kusindikwa.

FAO inasema mara nyingi mabadiliko hayo hutokana na kubadili mfumo wa maisha, na kwa ukanda huo kumekuwa na ongezeko ya matumizi ya vyakula vyenye ukari, mafuta ya wanyama na mbogamboga, na kiwango cha matumizi ya nafaka kimepungua.

Photo Credit
Picha: FAO