Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utapiamlo una waathiri watoto wa Sudan

Utapiamlo una waathiri watoto wa Sudan

Njaa na utapiamlo unaenea kwa viwango vya kutisha nchini Sudan huku takribani watoto milioni 3.6 wakikakabiliwa na utapiamlo. Wataalamu wa lishe huko Darfur Kaskazini wanaendelea kusaidia familia kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wake. Hata hivyo suluhisho la uhakika ni usitishaji wa mapigano ili kuweza kuruhusu misaada ya kibinadamu kufikia wote wenye uhitaji. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Bosco Cosmas

Taarifa ya Bosco Cosmas

Hali ya lishe kwa watoto ni ngumu sana katika maeneo mengi ya Darfur Kaskazini nchini Sudan kutokana na mzozo unaoendelea nchini humo pamoja na hali mbaya ya kiuchumi jambo linalowaweka watoto mtegoni, kupata magonjwa ya lishe ikiwemo utapiamlo. UNICEF na wadau wengine wa afya, wanafanya kazi kuhakikisha watoto wanapata tiba stahiki.

Halima ni mtaalamu wa lishe huko kitongoji cha Tawila, Darfur kaskazini anasimulia hali ilivyo

HALIMA – Sabrina

Nimefanya kazi katika masuala ya lishe tangu mwaka 2017. Watoto wanasumbuliwa sana na utapiamlo. Hakuna chakula cha kutosha kutokana na ugumu wa maisha wanaopitia familia nyingi za Darfur, familia hazina pesa ya kutosha kununua aina mbalimbali za vyakula, kwahiyo mtoto anaweza aina moja tu ya kwa mwezi mzima kama vile, uji. Hakuna matunda wala mboga mboga ama kitu chochote jambo linalosababisha utapiamlo.”

Mbali na changamoto wazipatazo watoto, Halima anaeleza magumu anayopitia katika utendaji kazi wake.

HALIMA – Sabrina

Ninafanya hii kazi ya kusaidia maisha ya Watoto, tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba hatujapokea mshahara wetu, hapa tupo wanne tu na tunafanya kazi usiku na mchana. Tunawapatia maziwa yenye virutubisho na pia matibabu kwa watoto wanaoharisha na kutapika na matibabu mengine ya kila siku. Hatuna vikonge wala majagi ya kutosha, tunatumia majagi ya kutengenezea maziwa, inaumiza sana kutokuwa na vitendea kazi hivi, iwapo hakutakuwa na chakula cha tiba wala maziwa ya tiba kwa ajili ya kuwapa hawa watoto itakuwa vigumu sana kuwapatia matibabu watoto hawa. Tunawafundisha wazazi hatua za kuchukua wawapo majumbani mwao na pia tunawafundisha kuhusu usafi na lishe. Tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha tunawapatia dawa na kuokoa maisha ya watoto huku tukiwa na matumaini kuwa watakuwa na afya njema na kupona utapiamlo”

UNICEF Pamoja na wadau wengine wa afya wanaendelea kusambaza misaada ya lishe kwa watoto wenye utapiamlo hata katika maeneo ya vita ili kuendelea kuokoa maisha ya watoto hao ambao wapo hatarini zaidi. Misaada hiyo inawanufaisha zaidi ya watoto 240,000 wenye utapiamlo, katika mji wa Darfur.

Pakua

Njaa na utapiamlo unaenea kwa viwango vya kutisha nchini Sudan huku takribani watoto milioni 3.6 wakikakabiliwa na utapiamlo. Wataalamu wa lishe huko Darfur Kaskazini wanaendelea kusaidia familia kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wake. Hata hivyo suluhisho la uhakika ni usitishaji wa mapigano ili kuweza kuruhusu misaada ya kibinadamu kufikia wote wenye uhitaji. 

Taarifa ya Bosco Cosmas

Hali ya lishe kwa watoto ni ngumu sana katika maeneo mengi ya Darfur Kaskazini nchini Sudan kutokana na mzozo unaoendelea nchini humo pamoja na hali mbaya ya kiuchumi jambo linalowaweka watoto mtegoni, kupata magonjwa ya lishe ikiwemo utapiamlo. UNICEF na wadau wengine wa afya, wanafanya kazi kuhakikisha watoto wanapata tiba stahiki.

Halima ni mtaalamu wa lishe huko kitongoji cha Tawila, Darfur kaskazini anasimulia hali ilivyo

HALIMA – Sabrina

Nimefanya kazi katika masuala ya lishe tangu mwaka 2017. Watoto wanasumbuliwa sana na utapiamlo. Hakuna chakula cha kutosha kutokana na ugumu wa maisha wanaopitia familia nyingi za Darfur, familia hazina pesa ya kutosha kununua aina mbalimbali za vyakula, kwahiyo mtoto anaweza aina moja tu ya kwa mwezi mzima kama vile, uji. Hakuna matunda wala mboga mboga ama kitu chochote jambo linalosababisha utapiamlo.”

Mbali na changamoto wazipatazo watoto, Halima anaeleza magumu anayopitia katika utendaji kazi wake.

HALIMA – Sabrina

Ninafanya hii kazi ya kusaidia maisha ya Watoto, tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba hatujapokea mshahara wetu, hapa tupo wanne tu na tunafanya kazi usiku na mchana. Tunawapatia maziwa yenye virutubisho na pia matibabu kwa watoto wanaoharisha na kutapika na matibabu mengine ya kila siku. Hatuna vikonge wala majagi ya kutosha, tunatumia majagi ya kutengenezea maziwa, inaumiza sana kutokuwa na vitendea kazi hivi, iwapo hakutakuwa na chakula cha tiba wala maziwa ya tiba kwa ajili ya kuwapa hawa watoto itakuwa vigumu sana kuwapatia matibabu watoto hawa. Tunawafundisha wazazi hatua za kuchukua wawapo majumbani mwao na pia tunawafundisha kuhusu usafi na lishe. Tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha tunawapatia dawa na kuokoa maisha ya watoto huku tukiwa na matumaini kuwa watakuwa na afya njema na kupona utapiamlo”

UNICEF Pamoja na wadau wengine wa afya wanaendelea kusambaza misaada ya lishe kwa watoto wenye utapiamlo hata katika maeneo ya vita ili kuendelea kuokoa maisha ya watoto hao ambao wapo hatarini zaidi. Misaada hiyo inawanufaisha zaidi ya watoto 240,000 wenye utapiamlo, katika mji wa Darfur.

Audio Credit
Leah Mushi / Bosco Cosmas
Sauti
1'58"
Photo Credit
© UNICEF/Mohamed Zakaria