Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS ziarani Nadiangere na uzinduzi wa shule ya msingi

UNMISS ziarani Nadiangere na uzinduzi wa shule ya msingi

Pakua

Ikiwa ni moja ya majukumu yake, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS wakishirikiana na mamlaka za mitaa za nchi hiyo umefanya ziara maalum katika Kijiji cha Nadiangere na kusikiliza kero za wananchi pamoja kuzindua shule mpya ya msingi. 

Ndege ya UNMISS ikiwa na timu ya walinda amani na wawakilishi kutoka serikali za mitaa inafika kijiji cha Nadiangere kilichoko katika jimbo la Equatorial Magharibi na kulakiwa kwa shamsham na wananchi wa kijiji hicho wakiamini msemo wa Kiswahili usemao “Mgeni njoo mwenyeji apone.” 

Katika mkutano wa pamoja, wananchi hao walieleza changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo ukosefu wa huduma za kimsingi kama viles hule, huduma za afya pamoja na usalama. 

Wananchi hao wakaeleza uhaba huu umechangiwa na kuwasili kwa wakimbizi wa ndano wanaokimbia kuzuka kwa vurugu za wenyewe kwa wenyewe hivi karibuni huko karibu na eneo la Tambura. 

Severina Angelo mwenye umri wa miaka 21, mama wa watoto wawili akapaza sauti.

“Tumechoka sana, tunahitaji amani, tumeshateseka sana. Tunahitaji shule, tunahitaji hospitali na vitu vingine vingi ambavyo tunakosa.”

Jane Lanyero Kony, Ni Mkuu wa Ofisi ya UNMISS kwa jiji la Yambio na anawaeleza wanakijiji hao kuwa “Subira yavuta heri.”

“Unajua sisi tuko hapa kusikiliza changamoto zenu ni zipi na kisha tunaporudi ofisini tunaenda kuangalia ni kwa kiwango gani tunaweza kuhamasisha upatikanaji wake miongoni mwa jumuiya ya Umoja wa Mataifa. Kama UNMISS, tunaendelea kufanya kile ambacho ni mamlaka yetu, ambacho ni, ulinzi wa raia. Tunaendelea kufanya kazi na serikali, ili kukamilisha juhudi zao za kulinda kila raia nchini Sudan Kusini.”

Mbali na kuwasikilisha wananchi pia wamezindua shule ya msingi iliyojengwa kwa ufadhili wa UNMISS katika eneo hilo. Shule hiyo ina vyumba vitatu vya madarasa, ofisi ya walimu, na inatoa mazingira bora ya kujifunzia kwa zaidi ya wasichana na wavulana 300.

Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
1'47"
Photo Credit
UNMISS/Nektarios Markogiannis