Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO: COVID-19 imerudisha nyuma muongo wa maendeleo ya umri wa watu kuishi

WHO: COVID-19 imerudisha nyuma muongo wa maendeleo ya umri wa watu kuishi

Pakua

Ripoti mpya ya Takwimu za Afya Ulimwenguni iliyotolewa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, inaonyesha kuwa janga la coronavirus">COVID-19 limebadilisha mwelekeo wa kuongezeka kwa umri wa watu kuishi wakati wa kuzaliwa na matarajio ya maisha yenye afya wakati wa kuzaliwa HALE.

Ripoti hiyo ya takwimu za afya ulimwenguni hutolewa kila mwaka na WHO ikijumuisha viashirikia vya afy na vinavyohusiana na imekuwa ikitolewa tangu mwaka 2005.

Ripoti yam waka huu kwa mujibu wa WHO imetathimini Zaidi ya viashiria 50 vinavyohusiana na afya kuanzia malengo ya maendeleo endelevu SDGs na mikakati kazi 13 ya WHO au GPW13.

Ripoti inasema Janga la COVID-19 limefuta karibu muongo mmoja wa maendeleo katika kuboresha umri wa watu kuishi ndani ya miaka miwili tu. Kati ya 2019 na 2021, umri wa kuishi duniani ulipungua kwa mwaka 1.8 hadi miaka 71.4 ukirejea nyuma hadi kiwango cha mwaka 2012.”

Pia ripoti imeongeza kuwa umri wa kuishi kwa afya duniani ulipungua kwa miaka 1.5 hadi miaka 61.9 mwaka 2021 ukiwa umerudi nyuma kwenye kiwango cha mwaka 2012. 

Ripoti hiyo ya 2024 pia imeainisha ni jinsi gani athari hizo zimehisiwa tofauti na hazilingani kote duniani.

Maeneo ya WHO yaliyoathirika Zaidi ripoti inasema ni Ukanda wa Amerika na Kusini-Mashariki mwa Asia, ambako umri wa kuishi ukishuka kwa takriban miaka 3 na matarajio ya maisha yenye afya yakishuka kwa miaka 2.5 kati ya mwaka 2019 na 2021.

Kinyume chake, Kanda za Pasifiki Magharibi zimeathiriwa kidogo wakati wa miaka miwili ya kwanza ya janga hla COVID-19 na kupata hasara ya chini ya miaka 0.1 katika umri wa kuishi na miaka 0.2 katika matarajio ya maisha yenye afya.

Audio Credit
Flora Nducha
Sauti
2'25"
Photo Credit
UNDP India