Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yakutana kujadilia changamoto zinazowakabili wahamiaji wakati wa machafuko

IOM yakutana kujadilia changamoto zinazowakabili wahamiaji wakati wa machafuko

Ripoti moja imesema kuwa kiasi cha wahamiaji 800,000 nchini Libya walikosa fursa muhimu na hivyo kulazimika kukimbia nchini humo kutokana na machafuko yaliyolikumba eneo hilo. Ama kumeelezwa pia ndani ya mwaka huu pekee kiasi kingine cha wahamiaji waliondoka nchini Syria ikiwa sehemu nyingine ya machafuko.

Kutokana mikwamo hiyo, maafisa wa ngazi za juu wa shirika la Umoja wa Mataifa wanaohusika na uhamiaji IOM wanaanza mkutano wao siku mbili mjini Geneva kujadilia namna dunia inavyoweza kuondokana na matukio ya namna hiyo.

Shabaha kubwa ya wajumbe kwenye mkutano huo ni kuangalia kwa kiasi gani jumuiya za kimataifa zinaweza kutoa msaada wa pekee kuwaepusha na madhara yoyote wahamiaji katika nchi zinazotumbukia kwenye mizozo.

Kuna malalalamiko ya mara kwa mara juu ya kusaulika kwa misaada ya kibanadamu katika maeneo yanayokumbwa na machafuko.