Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya Kimataifa juu ya uhalifu yaweka hadharani nyaraka zilizokuwa nyeti

Mahakama ya Kimataifa juu ya uhalifu yaweka hadharani nyaraka zilizokuwa nyeti

Mahakama ya kimataifa iliyoendesha kesi dhidi ya uhalifu wa kivita nchini Cambodia uliotendeka wakati wa utawala la Khmer Rouge imezitoa hadharani nyaraka zaidi ya 1,700 ambazo hapo awali zilichukuliwa kama nyaraka nyeti na kuwekwa kama sili.

Mahakama hiyo imeamuru nyaraka hizo ambazo pia zinajumuisha mwenendo wa kesi na ushahidi uliokuwa ukitolewa na waathirika wa maauji hayo, ziwekwe hadharani ili jamii ipate kuzisoma.

Katika taarifa yake, mahakama hiyo imesema kuwa hatua hiyo imefikia baada ya kufanyika uhakika wa kina na mahakama kujiridhisha kuwa nyaraka hizo zinaweza kuwekwa hadharani

Machafuko na maisha ya uhasama yaliyoshuhudiwa wakati wa utawala wa Khmer Rouge yalisababisha watu zaidi ya milioni mbili walipoteza maisha