Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM washerekea Mji Mkuu wa Australia kuweka vipaumbele vya kukabiliana na majanga ya kimazingira

UM washerekea Mji Mkuu wa Australia kuweka vipaumbele vya kukabiliana na majanga ya kimazingira

Umoja wa Mataifa umeutaja mji mkuu wa Australia kuwa ni miongomi mwa majiji machache duniani ambayo inatizamwa kama kioo cha kutokana na kuwa na mifumo inayotambua suala la kukabili tukio la dharura.

Mji huo ambao unakabiliwa na matukio ya majanga ya kimazingira kama mafuruko ya mara kwa mara, matukio ya kuzuka kwa moto katika misitu na kuanguka kwa barafu kumefanya mji huo wa Canberra kuanzisha mpango mkakati unaotupia jicho eneo la kuwa tayari kukabili majanga.

Akizungumza katika kongamano la kimataifa la sita linaloangazia hali ya miji kongamano ambalo linafanyika mjini Naples, Italia, Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kitendo cha kukabili majanga ya dharura Margareta Wahlström amesifu juhudi zilizoanzishwa na mji huo.

Amesema kuwa mji huo sasa anachukua nafasi kubwa ya ushawishi kwa miji mingine ambayo amesema inapaswa kuiga toka kwa mji huo kuandaa mazingira yanayoweza kukabiliana na majanga ya kimazingira.