Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yaorodhesha Kanisa la Kiasili na barabara ya mahujaji Bethlehem kwenye maeneo ya urithi

UNESCO yaorodhesha Kanisa la Kiasili na barabara ya mahujaji Bethlehem kwenye maeneo ya urithi

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, limeorodhesha Kanisa la Kiasili, ambako alizaliwa Yesu, na barabara ya mahujaji iliyopo mji wa Bethlehem, Palestina, kama maeneo ya urithi wa kiasili.

Maeneo mengine ambayo yameorodheshwa na UNESCO yanapatikana Israel, Palau, Indonesia na mji wa Rabat, Morocco. Maandishi maalum yanaendelea kuwekwa kwa ajili ya utambuzi huu. UNESCO pia imeliweka Kanisa la Kiasili na barabara ya mahujaji ya Bethlehem kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa kiasili yaliyomo hatarini, kwa sababu linaharibiwa na maji yanayovuja.

Haya yote yamefanyika katika mkutano wa Kamati ya Urithi wa Kiasili, inayokutana mjini St. Petersburg hadi tarehe sita Julai.