Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya Vifo na Majeraha yapungua nchini Afghanistan mwaka huu:UM

Idadi ya Vifo na Majeraha yapungua nchini Afghanistan mwaka huu:UM

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan umesema kuwa idadi ya watu waliouawa kwa kipindi cha miezi minne ya mwaka huu ilipungua kwa asilimia 21 ikilinganishwa na ya kipindi kama hicho mwaka uliopita nchini Afghanistan.

Kulingana na utafiti uliondeshwa na idara ya haki za binadamu kwenye ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA niwa kuwa raia 579 waliuawa huku 1,216 wakijeruhiwa toka tarehe mosi mwezi Januari hadi 30 mwezi Aprilki mwa huu.

Akihutubia waandishi wa habari mjini Kabul Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa UNAMA Jan Kubis anasema kuwa vifo vya raia vinatokea kwa viwango ambavyo havitakubalika. Ameongeza kuwa makundi yanayoipinga serikali hayawaeshimu raia akisema kuwa kutumika kwa mabomu ya kutegwa ardhini na washambulizi wa kujitoa mhanga ni suala ambalo halitakubalika.