Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugiriki, Yugoslavia ya zamani zakutana New York kwa majadiliano ya eneo

Ugiriki, Yugoslavia ya zamani zakutana New York kwa majadiliano ya eneo

Pande zinazozozana juu ya mpaka wa eneo baina ya Ugiriki na Jamhuri ya zamani ya Yugoslavia ya Mecedonia zimekamilusha dura ya kwanza ya majadiliano yenye shabaha ya kuleta suluhu kuhusuaana na mzozo wa jina gani liwe rasmi kuhusiana na pande hizo mbili.

Umoja wa Mataifa ndiyo uliosimamia majadiliano hayo ambayo yamewaleta pamoja wawakilishi toka pande zote mbili waliojadiliana kwa marefu juu ya hatua za kuuleta kwenye ukomo mzozo huo.

Kulingana na msimamizi wa majadiliano hayo Bwana Matthew Nimetz pande hizo zilizokutana mjini New York kimsingi zimeafikiana kuweka makusudia ambayo yatautuliza mkwamo huo. Hata hivyo ili kurahisisha majadiliano hayo, pande zote mbili kwanza zilikuwa na majadiliano ya faragha na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa aliyeratibu mazungumzo hayo.