Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO kutoa msaada wa kitaalamu kwa nchi kadhaa

UNESCO kutoa msaada wa kitaalamu kwa nchi kadhaa

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO limeandaa mpango maalumu wa kitaalamu ambao unatazamia kuzifaidia nchi kadhaa.

UNESCO imesema kuwa mpango wa utoaji wa msaada wa kitaalamu unatazamiwa kuzifaidia nchi za Burkina Faso, Cambodia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya  Congo, Seychelles na Viet Nam. Mpango huo unakusudia kuziwezesha nchi hizo kupata msaada wa kitaalamu katika maeneo ya ujenzi wa sera, mienendo ya kisiasa pamoja na ujasiliamali.

Nchi husika zimeridhia mpango huo na zimeelezea utayari wao wa kuanza kutekeleza mipango ya kimaendeleo.