Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Syria itaheheshimu pendekezo kutoka nchi za kiarabu:Ban

Syria itaheheshimu pendekezo kutoka nchi za kiarabu:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anasema kuwa ana matumaini kwamba mpango mpya wa amani uliopendekezwa na muungano wa nchi za kiarabu umetekelezwa ili kumaliza mauaji yanayoendelea nchini Syria.

Ban aliyasema hayo alipofanya ziara ya kisiri kwenye mji mkuu wa Libya Tripoli akiandamana na rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser. Ripoti zinasema kuwa Syria imekubali mpango uliopendekezwa na muungano wa nchi za kiarabu unaojumuisha kuachiliwa huru kwa wafungwa, kuondolewa wanajeshi mitaani na mazungumzo kati ya serikali na upinzani.