Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

09 Agosti 2024

09 Agosti 2024

Pakua

Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Flora Nducha akimulika watu wa jamii ya asili, mtoto kunyonyeshwa maziwa ya mama, matumizi ya magunzi ya msonobari kutengeneza mboji salama na mashinani ni  ujumbe wa mshairi mashuhuri duniani kutoka nchini Marekani.

  1. Kulinda haki za watu wa jamii ya asili za kujitenga kwa ridhaa na kuishi maeneo yao asili ndio ujumbe wa mwaka huu wa siku ya kimataifa ya watu wa jamii ya asili dunia, ujumbe ambao Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni sahihi na kila mtu anapaswa kuuzingatia.
  2. Afisa wa UNICEF nchini Tanzania akionesha kivitendo kile wanachohamasisha kwa akina mama yaani kunyonyesha watoto wao maziwa ya mama pindi wanapojifungua.
  3. Katika makala, Assumpta Massoi anamulika ni kwa vipi magunzi ya mbegu za msonobari yamegeuka lulu huko Tunisia na kuwa chanzo cha kipato kwa mhitimu wa Chuo Kikuu aliyekaa miaka 6 bila ajira.
  4. Ujumbe wa mshairi Amanda Gorman kuhusu vita inayoendelea huko Gaza na madhara yake kwa watoto.
Sauti
10'46"