Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 yazidisha mzigo  kwa wanawake kusimamia familia Uganda

COVID-19 yazidisha mzigo  kwa wanawake kusimamia familia Uganda

Pakua

Mlipuko wa virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 umeweka wazi mambo mengi ambayo yanaendelea katika jamii. Mifumo ya kiafya ya nchi mbalimbali, usawa wa kijinsia, uchumi na hata uwezo wa kukabiliana na majanga.  Nchini Uganda hususani maeneo ya magharibi na katikati mwa nchi licha ya wanawake kuwa na jukumu muhimu la kuhudumia familia hususani katika suala la chakula, lakini mtazamo wa jamii juu ya wanawake unawabana katika masuala kadhaa ambayo yamenasibishwa na uanaume zaidi. Mathalani katika kipindi hiki mabcho magari yamewekewa vizuizi vya kutembea, ni changamoto kubwa kwa wanawake wa maeneo ambayo jamii ina mtazamo hasi kwa mwanamke kuendesha pikipiki au baiskeli. Kuhusu hali hiyo, mwandishi wetu John Kibego amemuhoji Bi Monica Kabakwonga, jiunge nao katika makala hii. 

Audio Credit
Loise Wairimu
Audio Duration
3'50"
Photo Credit
WFP/Marco Frattini