Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Joram Nkumbi na Vivian Joseph: Vijana wa Afrika lazima tuchangamkie fursa na kujifunza toka kwa wenzetu

Joram Nkumbi na Vivian Joseph: Vijana wa Afrika lazima tuchangamkie fursa na kujifunza toka kwa wenzetu

Jukwaa la vijana la Baraza la kiuchumi na kijamii ECOSOC limekunja jamvi jana jioni hapa makaomakuu ya Umoja wa Mataifa ambapo zaidi ya vijana 1000 kutoka nchi zaidi ya 80 wameshiriki wakiwemo Vivian Joseph Afisa tabibu akiwasilisha vijana katika jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC na Joramu Nkumbi mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la Afrika la viongozi vijana kwa upande wa Tanzania. 

Akizungumza na Flora Nducha wa UN News Joramu Nkumbi ameweleza alichojifunza “kwanza nilikuwa na shauku kubwa sana ya kutaka kujua endapo vijana wengine wanaotoka mabara tofauti na Afrika wanawazana kufikiria vipi? Je wanafikiri kama vijana wa Afrika tunavyofikiri. Na kwa kweli nimeona hawatofautiani sana na sisi.”

Ameendelea kusema kuwa na pia “Changamoto wanaozipitia katika nchi zao ni kama zilezile tu kama vile wanapohitimu vyuo vikuu kujaribu kupata shughuli wanazohitaji, au kupata ajira ni mtihani mkubwa , changamoto za mabadiliko ya tabianchi na mataifa baadhi ya Amerika Kusini kukosekana kwa Amani bado kunaendelea .”

Joramu Nkumbi mkurugenzi mtendaji wa Jukwaa la viongozi vijana Afrika kwa upande wa Tanania akizungumza na UN News Kiswahili wakati wa jukwaa la vijana la ECCOSOC
UN News/Assumpta Massoi
Joramu Nkumbi mkurugenzi mtendaji wa Jukwaa la viongozi vijana Afrika kwa upande wa Tanania akizungumza na UN News Kiswahili wakati wa jukwaa la vijana la ECCOSOC

Malalamiko ya vijana dhidi ya serikali

Joramu amesema kitu kingine ambacho amejifunza ni kwamba pia vinjana wa mataifa mengine “Wamekuwa wakilalamika hawaridhishwi na serikali zao na kuna kitu zaidi wanataka kifanyike.”

Lakini kikubwa zaidi kulichomfurahisha Joramu ni vijna kujitambua na kutambua jukumu lao katika jamii.

“Pia nimependa namna ambavyo vijana wameona kwamba wao ni sehemu ya kutatua hizo changamoto ziwe za mabadiliko ya tabianchi, za mazingira, za kisiasa, za amani, za ajira na kuona kwamba wanatakiwa kuwa msitari wa mbele.”

Pia amesema endapo kuna maazimio ambayo ymepitishwa na Umoja wa Mataifa basi hiyo ni fursa ya vijana kuyatumia illi kushinikiza serikali zao kufanya mabadiliko kwa kuziambia tunahitaji mabo haya.

Vivian Joseph mtabibu na mkuu wa kitengo cha afya akiwakilisha vijana wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC akizungumza na UN News
UN News/Assumpta Massoi
Vivian Joseph mtabibu na mkuu wa kitengo cha afya akiwakilisha vijana wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC akizungumza na UN News

Je ni kipi mtaenda nacho nyumbani kwa vijana wenzenu

Viviane amesema “Kwanza ni masuala mazima ambavyo Dunia inakwenda kwa kasi hasa kwa vijana wenyewe , kwani vijana wa mataifa mengine wameamka kwa kiasi kikubwa.”

Ameongeza kuwa moja ya vitu ambavyo vinawasaidia na kuwachagiza ni “Kuweza kupokea ushirikiano baina yao na serikali zao kwa kuwapa fursa za kuweza kujifunza kwenye majukwaa kama haya.”

Pia amesema kutambua umuhimu wa teknolojia na kuitumia vyema ni jambo la msingi sana kwa vijana.

Mfano amesema kutumia fursa hizo za kidijitali “Katika masuala mazima ya mazingira, masuala ya tabianchi, masuala ya kiuchumi , masuala ya ajira ni jambo ambalo tukirejea nyumbani itakuwa sehemu ya kuwakumbusha vijana wenzetu.”

Kutumia fursa za mtandao vyema

Vivian amesema watatumia walichojifunza kwa wenzao kuhusu mitandao na kuwashawishi vijana wenzao kukumbatia fursa zake “Kwa vina wale ambao wana fursa ya mitanfdao ya intaneti basi aweze kuzitumia vyema fursa hizo zilizopo kuongeza maarifa , kujifunza zaidi maarifa ya teknolojia ili tuweze kuendana na kasi ya dunia inavyokwenda.”

 

Pakua
Audio Credit
Leah Mushi/Flora Nducha
Audio Duration
3'19"
Photo Credit
UN News/Assumpta Massoi