Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres: Tumieni vizuri Mjadala wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu kuhusu ufadhili wa maendeleo

Guterres: Tumieni vizuri Mjadala wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu kuhusu ufadhili wa maendeleo

Pakua

Viongozi wa ulimengu wanaohudhuria Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wamefanya Mjadala wa Ngazi ya Juu kujadili ufadhili kwa ajili ya maendeleo ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewasihi kuitumia fursa ya majadiliano haya ili kufanya marekebisho katika mfumo wa ufadhili duniani. Evarist Mapesa na taarifa zaidi.

“Waheshimiwa, Mabibi na mabwana…Katika masuala yote tutakayojadili wiki hii, ufadhili unaweza kuwa muhimu zaidi.” Ndivyo alivyoanza hotuba yake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mbele ya viongozi wa ulimwengu kwa lengo la kutafuta suluhisho la ufadhili wa maendeleo unaosuasua duniani. 

Akitumia mfano wa nishati isukumavyo mitambo, Guterres amesema kwa sababu ufadhili wa maendeleo ndio nishati inayosukuma maendeleo kwenye Ajenda ya mwaka 2030 na Mkataba wa Paris. Leo, nishati hiyo inaisha na injini ya maendeleo endelevu inadumaa, inakwama, na inarudi nyuma.

Bwana Guterres ameweka wazi kuwa kuna mgawanyiko mkubwa na unaokua kati ya nchi ambazo zinaweza kupata ufadhili kwa masharti yanayokubalika na zile ambazo haziwezi na zinaachwa nyuma zaidi akitoa mfano mchungu kwamba nchini zinazoendelea zinakabiliwa na gharama za kukopa hadi mara nane zaidi ya nchi zilizoendelea – kitu ambacho amekiita mtego wa madeni na hapo akatoa wito,

“Ninakuombeni mtumie mjadala huu wa ngazi ya juu kama jukwaa la ushirikiano wenye kujenga, kwa kuzingatia suluhisho za ufadhili za kiubunifu na vitendo ambazo zinaweza kuendelezwa katika miezi na miaka ijayo.”

Audio Credit
Evarist Mapesa
Sauti
1'41"
Photo Credit
UN Photo/Cia Pak