Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii ilinishangaa nilipoamua kusomea kuchomelea vyuma sababu mimi ni msichana

Jamii ilinishangaa nilipoamua kusomea kuchomelea vyuma sababu mimi ni msichana

Pakua

Tatizo la ajira hususan kwa vijana ni suala linaloumiza vichwa kuanzia ngazi ya familia, kitaifa mpaka kimataifa. Nchini kenya katika kusaka suluhu ya tatizo hili Serikali ya Kenya imeanzisha mradi wa Ajira na Fursa kwa vijana au KYEOP unaofadhiliwa na Benki ya Dunia ukilenga vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 mpaka 29 ambao wanapatiwa fursa ya elimu ili waweze kuajirika au wakishahitimu na kufungua biashara zao waweze kutengeneza fursa za ajira kwao na kwa wengine.

Msichana Esther Karisa ni mnufaika wa mradi wa KYEOP lakini yeye baada ya kujiunga na programu hiyo aliamua kusomea ufundi stadi wa kuchomelea vyuma au welding kwa lugha ya kiingereza, taaluma ambayo inaaminika ni ya wanaume pekee. Tusikie akisimulizi safari yake.

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
4'
Photo Credit
Benki ya Dunia