Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nukta Fakti na elimu kuhusu habari za uongo mtandaoni

Nukta Fakti na elimu kuhusu habari za uongo mtandaoni

Pakua

Janga la Corona au COVID-19 lilipoibuka miaka miwili iliyopita halikuleta changamoto za afya pekee bali kiuchumu na masuala mengine ya kijamii kama hofu juu ya taarifa zihusianazo na janga hilo. Kwakuwa janga hilo lilikuwa jipya wananchi wengi walijikuta wakihamaki kutokana na kuenea kwa taarifa za uzushi zilizokuwa zikisambaa mitandaoni.

Kwa kuona adha hiyo Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Umma wa Umoja wa Mataifa Melissa Fleming alizindua kampeni maalum ya “Tafakari kwanza” au “Verified initiative” kwa lengo la kuwataka watu kote duniani kutafakari kabla ya kusambaza taarifa au maudhui kwenye mitandao ya kijamii.

Wadau mbalimbali duniani waliunga mkono kampeni hiyo na nchini Tanzania kijana Nuzulack Dausen ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Nukta Afrika yenye lengo la kuelimisha waandishi wa habari naye alianzisha ukurasa maalum wa Nukta Fakti mtandaoni ambao unatoa elimu na kukanusha taarifa za uongo zinazoenea mitandaoni.

Dausen anatoa elimu ya namna mwananchi wa kawaida anavyoweza kutambua habari ya uongo mtandaoni.

Audio Credit
Assumpta Massoi/ Nuzulack Dausen
Audio Duration
4'8"
Photo Credit
Unsplash/Redgirl Lee