Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake katika sanaa wanakumbana na changamoto. Vijana wasiendekeze starehe – Mama Kayai

Wanawake katika sanaa wanakumbana na changamoto. Vijana wasiendekeze starehe – Mama Kayai

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, linasema sanaa ianawaleta watu karibu. Sanaa kama vile uigizaji, uchoraji, muziki mathalani wa mababu huzungumza mengi juu ya historia ya ustaarabu na uhusiano unaowaunganisha. 

Inawafanya watu wahisi na kuelewa ni nini kinachounganisha ubinadamu katika utofauti wa tamaduni zake na  hivyo kuchangia katika mustakabali wetu mzuri na endelevu.

Kuliangazia hilo, tunaelekea nchini Kenya ambako, Mary Kavere maarufu kama Mama Kayai ni muigizaji wa miaka mingi nchini Kenya na mmoja wa waasisi wa vipindi vya uigizaji nchini Kenya akiwa ameshriki katika vipindi vya radio na televisheni kwa karibu miaka 40. Mwaka 2018 alitunukiwa tuzo ya heshima kwa mchango wake katika fani ya uigizaji inayofahamika kama Grand Warrior Award. Kuanzia mwaka 1985 alishiriki kwenye kipindi cha VITIMBI kilichopeperushwa na shirika la utangazaji la serikali la Kenya, KBC na baadaye kwenye kipindi maarufu cha Vioja Mahakamani. Pia ameburudisha kwenye hafla kuu zikiwemo za serikali.  Mama Kayai amezungumza na mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi.

Audio Credit
Anold Kayanda/Jason Nyakundi
Audio Duration
4'9"
Photo Credit
Maktaba