Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za watoto zilindwe ili kulifikia lengo namba 3 na 4 la Malengo ya Maendeleo Endelevu

Haki za watoto zilindwe ili kulifikia lengo namba 3 na 4 la Malengo ya Maendeleo Endelevu

Pakua

Lengo namba 3 la Maendeleo Endelevu linalenga afya na ustawi bora kwa jamii wakati lengo namba 4 likilenga elimu bora. Malengo haya kwa namna nyingine yanasaidia kulifikia lengo namba 5 ambalo linasisitiza usawa wa kijinsia na hata kuweza kulifikia lengo namba 11 linalolenga kuwa na jamii endelevu ifikapo mwaka 2030. Wadau wa haki za watoto wanasema ili kufanikiwa na kupata matunda ya malengo haya na mengine, ni muhimu kujali haki za watoto ili kupata kizazi bora cha siku za usoni ingawa safari hiyo bado ni ndefu kwani katika jamii bado kuna vitendo vinavyowanyima watoto fursa hiyo. John Kabambala kutoka redio washirika Kids Time FM ameliangazia suala hili kwa kuzungumza na wadau watetezi wa haki za binadamu na kwanza ni Joel Festo, Mwenyekiti wa Baraza wa Baraza la Watoto Tanzania.

Audio Credit
Loise Wairimu\John Kabambala
Sauti
3'11"
Photo Credit
UN-Habitat/Kirsten Milhahn