Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ana kwa ana na Bi. Ida Odinga

Ana kwa ana na Bi. Ida Odinga

Pakua

Wanawake viongozi katika nchi nyingi, huangaliwa na jicho la kipekee na umma kwani wanashikiliwa kwa viwango vya juu zaidi kuliko wanaume. Lakini licha ya hali hiyo wanawake bado wanachukua nafasi mbali mbali iwe ni katika vyeo vya uongozi au katika jamii kwa ajili ya kuleta mabadiliko kwenye jamii zao.

Nchini Kenya mwanamke mmoja, Ida Odinga almaarufu Mama Ida anachagiza wasichana kwa ajili ya kuwatia moyo na kuwapa muongozo katika jamii ili kuwawezesha kujenga mustkabali bora katika siku za usoni.

Bi. Odinga ambaye ni mke wa mwanasiasa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga amezungumza na Grace Kaneiya wa Idhaa hii na kutoa fursa ya kumfahamu zaidi. Ungana naye. 

Audio Duration
3'50"
Photo Credit
UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya