Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yachukua hatua kukabili majanga ya asili

Tanzania yachukua hatua kukabili majanga ya asili

Pakua

Utabiri sahihi wa hali ya hewa ni mojawapo wa nyenzo  muhimu zinazoweza kuokoa maisha na pia kuepusha madhara makubwa yatokanayo na uharibifu wa miundombinu baada ya vimbuga na mafuriko.

Katika malengo ya maendeleo endelevu ,SDGs au ajenda 2030 ,  lengo namba 13 linahimiza serikali na mashirika mbalimbali kuchukua hatua za haraka ambazo zinaweza kukabiliana na madhara ya  mabadiliko ya tabianchi.

Nchini Tanzania, tayari hatua zinachukuliwa kwa kuwekeza katika sekta ya utabiri wa hali ya hewa , kwa kununua vifaa vya kisasa na pia elimu katika baadhi ya Vyuo Vikuu kuhusu utabiri huo kama anavyoelezea Dkt Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini  Tanzania alipozungumza na Patrick Newman wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa hivi karibuni alipokuwepo kikazi jijini New York, Marekani.

Audio Credit
Patrick Newman/ Grace Kaneiya
Audio Duration
2'58"
Photo Credit
UN News/Patrick Newman