Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upendo wa kweli sio lazima utoke kwa ndugu wa damu

Upendo wa kweli sio lazima utoke kwa ndugu wa damu

Jumuiko la vijana mwaka huu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, UN, lilisheheni shughuli mbalimbali zikiwemo mdahalo wa vijana na viongozi waandamizi wa UN, maonyesho na burudani kutoka kwa waimbaji mbalimbali.

Miongoni mwao ni Emmanuel Kelly ambaye ni mlemavu wa viungo, na mmoja kati ya vijana waliohutubia kwenye mkutano huo alikuwa kivutio kikubwa  wakati alizungumzia mambo mbalimbali kuhusu safari ya maisha yake binfasi . 

Mwandishi wetu Patrick Newman anatuletea makala ya historia na pia burudani ya  kijana Kelly  ambaye hakuficha hisia zake pindi alipofunguka kwa undani  kuhusu kilichopelekea mafanikio yake.

Muziki....

Hapa  ni ndani ya moja ya kumbi za mikutano kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani, shughuli ni mdahalo wa vijana..

Muziki..

Jukwaa lina taa zilizofifia zikiashiria burudani kando ya mdahalo…. Vigelegele na shangwe vinasikika na kijana Emmanuel Kelly  anatokea jukwaani akiwa amevalia suruali ya buluu, fulana nyeupe na kotijeusi la Ngozi.

Muziki...

Emmanuel ambaye ni mlemavu wa viungo anaanza kwa kuwahadithia wageni waalikwa maisha yake nchini Iraq ambako alitelekezwa kwenye boksi na kuokolewa na hatimaye kupelekwa kwenye kituo cha watoto yatima.

Mmiliki mwenye kituo hicho cha yatima alimpigia simu mwanamke mmoja aje amchukue Emmanuel na mwenzake! Mwanamke huyo aitwaye Moira Kelly sasa ndiye mama wa kambo wa Emmanuel.

Muziki...

Sauti ya Emmanuel

Alipofika  nilikuwa nimesubiri kwa siku 3 ili aje kutuokoa . kilichonipa hamasa  nilipokuwa Iraki nilijua nikipata fursa ya kuishi kwa siku nyingine moja tu basi inatosha kuniokoa, kwasababu nilikuwa na  talanta au kipaji ambacho ni  matumani,ujasiri na moyo wa kuthubutu.

 Akiwa katika hisia kali, Emmanuel akasema…..

Sauti ya Emmanuel

Kabla hatujaondoka  Kaka yangu akamuuliza je waweza kutusaidia mimi na Emmanuel? Na Moiraakajibu nitajaribu kadri niwezavyo.

 Wakati ukimbi mzima ukiwa   kimya, Emmanuel akaenda mbali zaidi na kusema

Muziki....

Sauti ya Emmanuel

kaka yangu akamsisitizia kwamba kama huwezi kutuchukuwa wote basi mchukuwe Emmanuel halafu utanifuata mimi baadaye ikiwezekana.

Muziki

Sauti ya Emmanuel

Kaka yangu tuliookolewa naye sio ndugu yangu wa damu ila toka siku hiyo ndio nikajua kwamba familia, upendo sio lazima awe ndugu wa damu. Kitu pekee kilicho na nguvu kuliko damu ni upendo. Tukifundisha ulimwengu na vijana upendo wa kweli tunaweza kubadili mustakabali wa histori ya dunia.

 Anasema kutokana na upendo huo yupo hapa hii leo

Kiitikio cha wimbo

Katika wimbo huu Emmanuel anasema…

Fungua macho yangu najua upo mbele yangu, fungua moyo wangu najua upo nami, katika maisha yangu najua upo pembeni nami kamwe sintokuwa peke yangu tena. Katika mawimbi najua ulinishika nikahisi mkono wa upendo, kila ulichokifanya kilibadili maisha yangu kamwe sintokuwa peke yangu.

Pakua

Jumuiko la vijana mwaka huu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, UN, lilisheheni shughuli mbalimbali zikiwemo mdahalo wa vijana na viongozi waandamizi wa UN, maonyesho na burudani kutoka kwa waimbaji mbalimbali.

Miongoni mwao ni Emmanuel Kelly ambaye ni mlemavu wa viungo, na mmoja kati ya vijana waliohutubia kwenye mkutano huo alikuwa kivutio kikubwa  wakati alizungumzia mambo mbalimbali kuhusu safari ya maisha yake binfasi .

Mwandishi wetu Patrick Newman anatuletea makala ya historia na pia burudani ya  kijana Kelly  ambaye hakuficha hisia zake pindi alipofunguka kwa undani  kuhusu kilichopelekea mafanikio yake.

Audio Credit
Patrick Newman
Audio Duration
4'29"
Photo Credit
Picha ya UN /Manuel Elias