Michezo ni daraja hata katika vita dhidi ya utumikishaji watoto
Katika kampeni ya kupiga vita utumikishwaji wa watoto kama askari katika maeneo ya migogoro ya vita inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNCEF, imeamua kugeukia michezo kufikisha ujumbe kutokana na uwezo wa michezokuunganisha watu.Uwakilishi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa ukaongeza nguvu katika kampeni hiyo kwa kuwaalika magwiji wastaafu wa kandanda waliowahi kuichezea ligi ya soka ya Ujerumani au Bundesliga kuja Umoja wa Mataifa kushiriki mechi kwa lengo la kuchagiza vijana na mashabiki wengine kuhusu kampeni hiyo.
Ujumbe uliobebwa na kampeni hiyo ni “nguvu ya michezo katika kuwaunganisha watu kuelekea kwenye kombe la Dunia litakalofanyika nchini Urusi.” Kombe hilo ambalo ni moja ya mikusanyiko mikubwa kabisa duniani inayowaleta pamoja mamilioni .
Mwandishi wetu Patrick Newman alipata fursa ya kufuatilia hafla ya kampeni hiyo ya kihistoria iliyoambatana na kabumbu kwa katika viwanja vya Umoja wa Mataifa . Ungana naye katika makala hii upate undani zaid