Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno "Simu" lina maana ngapi?

Neno "Simu" lina maana ngapi?

Pakua

Tujifunze Kiswahili, je wafahamu neno "Simulina maana ngapi? Ungana na mchambuzi wetu Onni Sigalla, mhariri mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la taifa nchini Tanzania BAKITA akizifafanua. 

Bwana Sigalla anasema neno "Simu" Lina maana zaidi ya moja, Mosi ni chombo kinachotumika kupeleka au kupokelea mawimbi ya Sauti, pili ni ujumbe au habari zinazopokelewa au simu ya upepo kama tunavyofahamu, tatu neno Simu ni ujumbe au habari yanayopokelewa kupitia mitambo maalum kama vile telegramu au fakisi, na maana ambayo watu wengi hawafahamu ni kwamba Simu ni samaki wadogo jamii ya dagaa.

Audio Credit
Onni Sigalla
Audio Duration
42"
Photo Credit
UN News Kiswahili