Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Samaki wametoweka kwasababu ya uvuvi haramu

Samaki wametoweka kwasababu ya uvuvi haramu

Pakua

Serikali nyingi duniani zimekuwa zikikabiliwa na changamoto za uvuvi haramu ambao mara nyingi huathiri mali asili ya baharini na kusababisha hasara kubwa kwa serikali, na pia  kuathiri mapato ya  wavuvi ambao hufuata sheria ya uvuvi.

Mwandishi wetu John kibego amefuatilia kwa ukaribu changamoto za uvuvi haramu katika ziwa Albert, katika wilaya ya Bulisa nchini Uganda ambapo wavuvi haramu wamekuwa wakivua kinyume cha sheria na kusababisha hasara kubwa katika mapato ya serikali ya kijiji.

Je nini kilichojiri ?ungana naye katika makala hii.

Audio Credit
Patrick Newman/ John Kibego
Audio Duration
3'35"
Photo Credit
Uvuvi bora sambamba na viwanda vya kuchakata samaki ni mojawapo ya mbinu za kuinua uchumi wa kaya na taifa kwa ujumla.