Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yatoa mafunzo ya kujikinga na UKIMWI kwa vijana nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na UKIMWI UNAIDS nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR linahamasisha jamii kupamba na na UKIMWI kwa kutoa elimu ya ngono salama kwa vijana. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Cecily Kariuki.

Taarifa ya Cecily Kariuki…

Takwimu za UNAIDS zinaonesha watu milioni 30.7 wanaoishi na Virusi vya UKIMWI - VVU sasa wanapata matibabu. Hii ni hatua kubwa katika afya ya umma ambayo pia imepunguza takriban nusu ya vifo vinavyohusiana na UKIMWI tangu mwaka 2010, kutoka zaidi ya milioni moja hadi 630,000 mwaka 2023.  

Hata hivyo vifo hivyo ni vingi ikilinganishwa na lengo la kuwa na vifo 250,000 ifikapo mwaka  2025.

UNAIDS wanasema mwaka 2023 kulikuwa na wastani wa maambukizi mapya ya VVU milioni 1.3 na takriban nusu ya walioambukizwa wanaishi mashariki na kusini mwa Afrika (35%) huku magharibi na Afrika ya kati wakiwa na maambukizi kwa asilimia 15%.

Ni kutokana na takwimu hizi ndio maana Mkurugenzi wa UNAIDS, nchini CAR Chris Fontaine akaona haja ya kutoa elimu kwa vijana.

Chris Fontaine – Bosco

“Vita na umaskini vimesababisha vifo vingi vya mapema nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, na matokeo yake, ni kuwa asilimia 78 ya idadi ya watu, ni chini ya umri wa miaka 35. Vijana hawa wanakabiliana na changamoto kubwa kupata elimu bora; kwa mfano, ni watu 4 kati ya 10 tu wa Kati ya Afrika ambao wanaweza kusoma na kuandika Ukosefu wa usawa wa kijinsia na ukatili wa kijinsia umewaacha wanawake katika hali hatarishi zaidi kwa VVU.”

Miongoni mwa waliopatiwa mafunzo katika Kituo cha Elimu kwa Afya ya Jinsia kwa Vijana, CISJEU ni Gniwali Ndangou.

Gniwali Ndangou - Sabrina

“Mimi ni yatima, ni mimi pekee kati ya ndugu zangu watatu ambaye ninapata matibabu kila siku na ninakunywa dawa bila kuacha. Ninaishi na VVU tangu nilipozaliwa. Zaidi ya mara moja, nilijaribu kujiua kwa kunywa vidonge.”

Gniwali Ndangou ambaye sasa ni mwalimu rika wa CISJEU amekuwa mstari wa mbele katika juhudi za kupambana na UKIMWI.

Topic: Afya

News tags: Afya kwa umma, UKIMWI, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, CISJEU

Partner: UNAIDS

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na UKIMWI UNAIDS nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR linahamasisha jamii kupamba na na UKIMWI kwa kutoa elimu ya ngono salama kwa vijana. 

(Taarifa ya Cecily Kariuki)

Takwimu za UNAIDS zinaonesha watu milioni 30.7 wanaoishi na Virusi vya UKIMWI - VVU sasa wanapata matibabu. Hii ni hatua kubwa katika afya ya umma ambayo pia imepunguza takriban nusu ya vifo vinavyohusiana na UKIMWI tangu mwaka 2010, kutoka zaidi ya milioni moja hadi 630,000 mwaka 2023.  

Hata hivyo vifo hivyo ni vingi ikilinganishwa na lengo la kuwa na vifo 250,000 ifikapo mwaka  2025.

UNAIDS wanasema mwaka 2023 kulikuwa na wastani wa maambukizi mapya ya VVU milioni 1.3 na takriban nusu ya walioambukizwa wanaishi mashariki na kusini mwa Afrika (35%) huku magharibi na Afrika ya kati wakiwa na maambukizi kwa asilimia 15%.

Ni kutokana na takwimu hizi ndio maana Mkurugenzi wa UNAIDS, nchini CAR Chris Fontaine akaona haja ya kutoa elimu kwa vijana.

Chris Fontaine – Bosco

“Vita na umaskini vimesababisha vifo vingi vya mapema nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, na matokeo yake, ni kuwa asilimia 78 ya idadi ya watu, ni chini ya umri wa miaka 35. Vijana hawa wanakabiliana na changamoto kubwa kupata elimu bora; kwa mfano, ni watu 4 kati ya 10 tu wa Kati ya Afrika ambao wanaweza kusoma na kuandika Ukosefu wa usawa wa kijinsia na ukatili wa kijinsia umewaacha wanawake katika hali hatarishi zaidi kwa VVU.”

Miongoni mwa waliopatiwa mafunzo katika Kituo cha Elimu kwa Afya ya Jinsia kwa Vijana, CISJEU ni Gniwali Ndangou.

Gniwali Ndangou - Sabrina

“Mimi ni yatima, ni mimi pekee kati ya ndugu zangu watatu ambaye ninapata matibabu kila siku na ninakunywa dawa bila kuacha. Ninaishi na VVU tangu nilipozaliwa. Zaidi ya mara moja, nilijaribu kujiua kwa kunywa vidonge.”

Gniwali Ndangou ambaye sasa ni mwalimu rika wa CISJEU amekuwa mstari wa mbele katika juhudi za kupambana na UKIMWI.

Audio Credit
Leah Mushi / Cecily Kariuki
Audio Duration
1'38"
Photo Credit
Public Health Alliance/Ukraine