Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamlaka kaskazini mwa Uganda zachukua hatua kutimiza SDGs kwa kulinda Tembo

Mamlaka kaskazini mwa Uganda zachukua hatua kutimiza SDGs kwa kulinda Tembo

Pakua

Ili kuunga mkono wito wa Malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs kama vile kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na wanyama na wakati huo huo binadamu nao wakipata uhakika wa chakula, mamlaka katika maeneo ya kaskazini mwa Uganda, zinachukua hatua ya kuwaelemisha wakazi wa maeneo hayo kuhusu jinsi ya kuishi kwa amani na wanyama kama vile tembo. Kutokana na ongezeko la idadi ya watu na uharibufu wa misitu ambayo ni makazi ya wanyamapori, mzozo kati ya binadamu na wanyamapori umekuwa ukiongezeka siku baada ya nyingine. Mzozo huo umeathiri uhakika wa chakula huku mzigo mkubwa ukiishia kwa wanawake wenye wajibu wa kitamaduni wa kusaka chakula katika jamii nyingi barani Africa. Mfano ni jamii ya Acholi kaskazini mwa Uganda hasa kwa majamii wa mbuga ya wanyamapori ya Murchichon Falls. Ili kufahamu kwa undani zaidi kuhusu changamoto wanazokumbana nazo, ungana na John Kibego katika makala ifuatayo. Kwanza ni Bi. Judith Nekesa kutoka wilayani Nwoya.
 

Audio Credit
Anold Kayanda/John Kibego
Audio Duration
4'
Photo Credit
UNEP GRID Arendal/Peter Prokosch