Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yapatia wakulima 200,000 Kenya stadi za kuhimili mabadiliko ya tabianchi

FAO yapatia wakulima 200,000 Kenya stadi za kuhimili mabadiliko ya tabianchi

Pakua

Nchini  Kenya mabadiliko ya tabianchi yamesababisha Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na serikali kusaidia wakulima, wafugaji na wavuvi kuweza kupata stadi mpya ili hatimaye waweze kunufaika na ufugaji, kilimo na uvuvi. Umoja wa Mataifa umechukua  hatua  hiyo kwa kutambua kuwa mabadiliko ya tabianchi yasiposimamiwa vyema yatasababisha umaskini kuongezeka sambamba na ukosefu wa chakula. Mathalani wakulima waliozoea kulima kwa kutegemea misimu ya hali ya hewa hivi sasa wamevurugwa kwa kuwa misimu hiyo haitabiriki tena. Viangazi vikali vinaleta ukame na hivyo umwagiliaji wa mashamba unakuwa wa shida. Hata hivyo shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kupitia miradi yake ya kupunguza makali ya madhara ya mabadiliko  ya tabianchi  limefikia wakulima 200,000 nchini Kenya kwa kuwapatia stadi. Je wanafanya nini? Assumpta Massoi anafafanua kwenye makala hii.

Audio Credit
Patrick Newman/ Assumpta Massoi/ Gabriel Rugalema
Audio Duration
4'6"
Photo Credit
FAO/Riccardo Gangale