Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana tumieni mitandao ya kijamii kusaka fursa na si kufuatilia watu- Marygoreth

Vijana tumieni mitandao ya kijamii kusaka fursa na si kufuatilia watu- Marygoreth

Pakua

“Vijana waache kutumia muda wao mwingi kufuatilia habari za watu maarufu mitandaoni bali watafute fursa za kuwanufaisha wao na jamii zao.”Ni maneno ya Marygoreth Richard mwandisih wa habari wa  Media Action ya shirika la utangazaji la Uingereza,  BBC ambaye  alishinda tuzo ya  kushiriki programu ya mwaka huu ya Reham Al Farah Memorial inayowanoa waandishi wa habari kuhusu masuala ya Umoja wa Mataifa.

 

Marygoreth alitoa kauli hiyo alipohojiwa na Grace Kaneiya wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani wakati akiwa makao makuu ya umoja huo kushiriki mafunzo hayo na alianza kwa   kueleza alivyoipokea nafasi hiyo ya kuiwakilisha nchi yake.

Audio Credit
Siraj Kalyango/Grace Kaneiya
Audio Duration
3'33"
Photo Credit
UN/Eskinder Debebe