Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

GAZA: Kutoka Gaza hadi Abu Dhabi kupata matibabu sahihi

GAZA: Kutoka Gaza hadi Abu Dhabi kupata matibabu sahihi

Pakua

Tangu kuanza kwa mzozo huko Ukanda wa Gaza mwezi Oktoba mwaka jana 2023 baina ya Israel na wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas mzozo ambao umesababisha vifo vingi, majeruhi, watu kupoteza kila kitu na wengine kutekwa, wiki iliyopita Ukanda huo umeshuhudia uhamisho mkubwa zaidi wa wagonjwa ambao wamepelekwa kupatiwa matibabu nje ya nchi.

Jumla ya wagonjwa na majeruhi walio mahututi 85 wamefanikiwa kuondolewa kutoka Ukanda wa Gaza kwenda Abu Dhambi katika Falme za kiarabu katika operesheni iliyotajwa kuwa “ngumu sana” iliyotekelezwa kwa ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO wakishirikiana na serikali ya Falme za kiarabu UAE pamoja na wadau wengine. Leah Mushi anatujuza zaidi katika makala haya.

Audio Credit
Flora Nducha/Leah Mushi
Sauti
4'32"
Photo Credit
© WHO