Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utipatipwa waongezeka miongoni mwa watoto barani Afrika

Utipatipwa waongezeka miongoni mwa watoto barani Afrika

Pakua

Utipwatipwa ni tatizo la afya la kimataifa na linalokua kwa kasi sana barani Afrika. Kati ya mwaka 2000 na 2016, idadi ya watu wazima wenye utipwatipwa au uzito wa kupindukia barani Afrika ilikaribia kuongezeka maradufu, na mwenendo huo huo sasa unaonekana kwa watoto. 

Cecily Kariuki wa Idhaa hii kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO amefuatilia kile ambacho mashirika ya Umoja wa MAtaifa na wadau wanafanya ili kukabiliana na changamoto hiyo ya kiafya duniani. Kwako Cecily!

Audio Credit
Cecily Kariuki
Sauti
3'28"
Photo Credit
© UNICEF/Bashir Ahmed Sujan