Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Benki ya Dunia

Jamii ilinishangaa nilipoamua kusomea kuchomelea vyuma sababu mimi ni msichana

Tatizo la ajira hususan kwa vijana ni suala linaloumiza vichwa kuanzia ngazi ya familia, kitaifa mpaka kimataifa. Nchini kenya katika kusaka suluhu ya tatizo hili Serikali ya Kenya imeanzisha mradi wa Ajira na Fursa kwa vijana au KYEOP unaofadhiliwa na Benki ya Dunia ukilenga vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 mpaka 29 ambao wanapatiwa fursa ya elimu ili waweze kuajirika au wakishahitimu na kufungua biashara zao waweze kutengeneza fursa za ajira kwao na kwa wengine.

Sauti
4'
UN News Kiswahili

Kunywa maziwa kuimarisha afya yako: FAO Tanzania

Tarehe 16 mwezi Oktoba kila mwaka dunia inaadhimisha siku ya chakula dunia, mwaka huu wa 2022 kauli mbiu ni Uzalishaji bora, lishe bora, mazingira bora, na maisha bora kwa wote :Habaki mtu nyuma” Kauli mbiu hii inaakisi hali halisi ya ulimwengu tunaoishi kwani kwa sasa kila pembe ya Dunia kuna changamoto mbalimbali kuanzia za mabadiliko ya tabia nchi mpaka vita vyote hivi vikipandisha bei za bidhaa na vyakula mara dufu na hii inasababisha jamii nyingi kujikuta hazina uhakika wa chakula.

Sauti
4'6"
UN NEWS/ Anold Kayanda

Nchi ya Somalia yaomba kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki

Nchi ya Somalia imeomba kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Dkt. Peter Mathuki alipokuwa hapa jijini New York Marekani ambapo alifanya mazungumzo na Leah Mushi wa idhaa hii.

Dkt. Mathuki anaanza kwakueleza jumuiya hiyo sasa ina wanachama wangapi. 

Sauti
2'25"
UN News

Kuhakikisha afya ya mtoto, Tanzania yatekeleza programu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto

Mashiriki 77 yasiyo ya kiserikali mkoani Morogoro, Tanzania yameanza kunufaika na mradi jumuishi wa kitaifa unaofahamika kwa kifupi MMMAM yaani Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto. Programu ya MMMAM inasimamiwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau kama  Shirika lisilo la kiserikali la Community Development Organization (CDO).

Kutoka Morogoro, Tanzania, Mwandishi Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM ya Morogoro Tanzania ametuandalia makala hii kuhusu mradi huo. 

 

Sauti
3'36"
UNCDF

UNCDF wamenipatia elimu na kuniunganisha na taasisi za kifedha – Mkurugenzi Nabuhima Foods  

Aaron Mwimo kwa jina la utani Joti, ni mmoja wa watu wanaochangia utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs kwa kuleta ustawi bora kwa jamii yake wilayani Kibondo, mkoa wa Kigoma nchini Tanzania.  

Bwana Mwimo alianzisha kiwanda kidogo cha kuchakata mazao ya wakulima kama vile mahindi na mihogo na akakipa kiwanda chake kidogo jina Nabuhima Food Supplies akisambaza unga katika mji eneo dogo la mji wa Kibondo hadi pale alipounganishwa na shirika la mitaji la Umoja wa Mataifa.  

Sauti
4'58"
UN News

Mwalimu Neema atengeneza vifaa vya kuwezesha watoto kuelewa anachofundisha.

Hii leo ni siku ya walimu duniani na ujumbe ni ujumbe marekebisho  ya mfumo wa elimu huanza na mwalimu. Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO linasema lengo la ujumbe huo  ni kusherehekea dhima muhimu ya walimu katika uwezo wa wanafunzi kwa kuhakikisha wana vifaa na mbinu zinazowawezesha za kujiwajibikia wao wenyewe na watu wengine.

Sauti
3'49"
CIFOR/Axel Fassio

Waandishi wa Habari Tanzania wajengewa uwezo kuhusu umiliki wa ardhi kwa wanawake

Mashirika mbalimbali ya kiraia nchini Tanzania yamezidi kuhamasika kuelimisha Jamii juu ya Haki ya Ardhi kwa wananchi, wanawake nikundi ambalo bado wameendelea kushindwa kumiliki ardhi hivyo inahitajika sauti ya pamoja katika utetezi wa Haki ya kumiliki Ardhi hususan katika mazingira magumu ya umasikini, mila na desturi kandamizi katika baadhi ya jamii.

Sauti
4'
UNICEF

Wanafunzi wapatiwa elimu ya namna ya kuishi na watu wenye ualbino

Mtoto umleavyo ndio akuavyo ni methali unaofundisha jamii kuhakikisha iwapo inataka watoto wawe na tabia fulani basi ni vyema waanze kuwafundisha wangali wadogo. Na ndicho kinachofanywa nchini Tanzania na Chama cha watu wenye ualbino TAS mkoa wa Morogoro, mashariki mwa taifa hilo. 

Chama hicho kinaendelesha programu ya kutoa elimu kwa wanafunzi na kimetembelea shule ya msingi kilakala iliyopo Manispaa ya Morogoro na kutoa elimu kwa wanafunzi wa darasa la sita na la saba juu ualbino na namna ya kuishi nao katika Jamii.

Sauti
3'23"
UN News

FAO Tanzania waadhimisha siku ya unywaji maziwa shuleni kwa kutoa maziwa kwa shule za msingi

Leo ni siku ya Kimataifa ya unywaji maziwa shuleni, siku inayopigiwa chepuo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo duniani FAO na kauli mbiu ya mwaka huu ni "Faulu Mtihani kwa glasi moja ya maziwa kila siku". FAO inasema unywaji wa kila siku wa kikombe cha maziwa ya ng’ombe cha ujazo wa mililita 200 humpatia mtoto mwenye umri wa miaka mitano asilimia 21 ya mahitaji ya protini na virutubisho vingine vya madini kama vile Kalsiamu, Magnesiamu na Vitamini. Kwa muj

Sauti
3'55"