Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

MINUSMA/Harandane Dicko

Tunashirikisha makundi mengi ili kuhakikisha utulivu Mali - MINUSMA 

Kuwalinda raia dhidi ya vitisho vya unyanyasaji wa kimwili ni kiini au kitovu cha kazi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Mali. Kwa ujumla, misheni sita za kulinda amani kwa sasa zimeidhinishwa, chini ya mamlaka ya Ulinzi wa Raia, kutumia njia zinazofaa kuzuia au kukabiliana na vitisho vya unyanyasaji dhidi ya raia, ndani ya uwezo na maeneo ya operesheni, na bila kuathiri jukumu la serikali mwenyeji.

Sauti
3'11"
UNFPA

Ugonjwa wa fistula unatibika. Mimi ni shuhuda - Magreth Rubeni

Leo tarehe 23 Mei 2022 ni Siku ya Kutokomeza Ugonjwa wa Fistula kauli mbiu yam waka huu ikiwa ni “Tokomeza Fistula, wekeza, imarisha ubora wa huduma za afya na wezesha jamii”. Ugonjwa wa Fistula ya uzazi huwapata wanawake wakati wa kujifungua hasa wale wanaojifungua wakiwa na umri mdogo pamoja na kukosa msaada stahiki wakati wa kujifungua, ambapo viungo kama kibovu cha mkojo na njia ya haja kubwa hujeruhiwa na  kusababisha mwanamke ashindwe kujizuia haja ndogo au kubwa. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani (WHO).

Sauti
9'3"
© UNICEF/Ashley Gilbertson

Vita ya Urusi na Ukraine imevuruga uchumi wangu – Abeid Aboubakar wa Dodoma, Tanzania 

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hivi karibuni akizungumza na Baraza la Usalama alitaka hatua zichukuliwe kukomesha vita alipokuwa akizungumzia namna ambavyo ni vita ni chachu kubwa ya njaa duniani kote.  

Vita ya hivi karibuni ambayo imeongeza chumvi katika jeraha ni kutokana na uvamizi wa Urusi kwa Ukraine ambao pamoja na madhara mengine kwa ulimwengu, imeathiri uzalishaji na usambazaji wa mafuta ambayo ni bidhaa mtambuka kwa mambo mengi na inapoyumba inayumbisha karibu mihimili yote ya uchumi.  

Sauti
4'13"
UPU

Mitandao ya kijamii inatusaidia lakini habari za uongo nazo ni changamoto - Kambini Lusenda, DRC

Takribani miaka miwili iliyopita, Umoja wa Mataifa ulizindua mkakati wake na ukapewa jina "iliyothibitishwa" au “Verified initiative” ambao unataka watu kote duniani kutafakari kabla ya kusambaza taarifa au maaudhi kwenye mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii ni moja ya njia inayotumiwa na jamii sio tu kwa mawasiliano kwa wapendwa wao bali pia kupata taarifa muhimu sehemu mbalimbali na za muhimu katika maisha ya kila siku.

Sauti
4'1"
United Nations

Unaelewa nini kuhusu “Usawa wa Kijinsia”? Baadhi ya vijana wanawake Tanzania wanaeleza

Umoja wa Mataifa unasema kuwa athari za kiuchumi na kijamii za janga la COVID-19 zimeathiri vibaya maendeleo ya hivi karibuni yaliyokuwa yamefikiwa katika usawa wa kijinsia. Unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana umeongezeka, ndoa za utotoni zinatarajiwa kuongezeka baada ya kuwa zimepungua katika miaka iliyopita. Gonjwa hilo limeonesha hitaji la hatua za haraka kushughulikia kukosekana kwa usawa wa kijinsia ambao bado umeenea ulimwenguni kote na umuhimu wa kurejea kwenye mbio za kufikia usawa wa kijinsia.

Sauti
4'49"
UN News/Thelma Mwadzaya

Chakula, elimu na maji ni mtihani mkubwa kwa waathirika wa ukame Turkana Kenya

Watu zaidi ya milioni 3 wameathirika vibaya na ukame nchini Kenya kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA huku eneo lililoathirika zaidi ni kaunti ya Turkana.

Maelfu ya watu wanahaha kupata mlo, Watoto imekuwa changamoto kwenda shule na maji ambayo ni uhai imekuwa bidhaa adimu kupatikana, sasa watu hao wanaililia jumuiya ya kimataifa kunyoosha mkono kunusuru uhai na maisha yao.

Sauti
5'37"
© UNOCHA

Mahitaji ya wakimbizi kambini Lusenda tunayatambua na tunayashughulikia

Wakimbizi katika kambi ya wakimbizi warundi ya Lusenda katika mkoa wa kivu ya Kusini mashariki mwa DRC, wametoa malalamiko yao mbele ya mkuu wa ofisi shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR katika ukanda wa kaskazini mashariki mwa DRC yenye makao yake mjini Goma. Jackie Keegan amepokea malalamiko hayo na kuahidi kuyafanyia kazi alipotembelea kambi hiyo. Mwandishi wetu nchini humo Byobe Malenga amefuatilia ziara hiyo na kutuandalia makala haya.

Sauti
3'53"
Warren Bright/UNFPA Tanzania

Ukatili wa kijinsia na uchumi vinachangia maambukizi ya VVU - Dreams Mbeya, Tanzania

Watekelezaji wa mradi wa Dreams  mkoani Mbeya nchini Tanzania, mradi unaowalenga vijana kati ya umri wa miaka kumi na tano hadi ishirini na nne walio kwenye hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI, VVU na walio ambao tayari wana virusi vya UKIMWI, wanasema kuwa baada ya kugundua kuwa ukatili wa kijinsia na hali ya uchumi vinachangia kwa kiasi kikubwa katika ueneaji wa mammbukizi ya VVU, ndipo waliamua kujikita na malengo kadhaa ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo  endelevu SDGs kama vile lengo namba 1 la kutokomeza umaskini, namba 3 kuhusu afya na ustawi bora na namba 5 la u

Sauti
4'33"