Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni muhimu vijana wawe makini na mitindo ya maisha ili isiathiri afya yao ya akili

Ni muhimu vijana wawe makini na mitindo ya maisha ili isiathiri afya yao ya akili

Pakua

Zama hubadilika na kupita, miaka ya nyuma iliwezekana kumuelezea mtu mwenye tatizo la afya ya akili kuwa amepatwa na hali hiyo kutokana na msongo wa mawazo, matumizi ya dawa za kulevya au ulevi wa pombe ulioptiliza, ingawaje pia wapo waliohusisha na imani za kishirikina.

Hata hivyo, tangu dunia ikumbatie utandawazi uliochangiwa na maendeleo ya teknolojia hasa upande wa habari na mawasiliano kwa kuanzishwa mitandao ya kijamii, teknolojia hiyo pamoja na mengi mazuri yake, sasa wataalamu wa afya wanaeleza kuwa kichocheo kimojawapo cha baadhi ya watu hususan kundi la vijana kupatwa na tatizo la afya ya akili baada ya muda mwingi kuwaza na kutumia mitandao hiyo ambapo inaelezwa inapofika hatua ya juu zaidi pasipo matibabu linaweza kumfanya mhusika kuwa kichaa

Ikiwa leo ni Siku ya Afya ya Akili Duniani ambayo huadhimishwa Oktoba 10 kila mwaka, Happiness Pallangyo wa redio washirika wetu Uhai FM ya Tabora Tanzania ameandaa makala hii akizungumza na wanajamii nchini Tanzania wakiwemo vijana na wataalamu wa afya ya akili kuhusu namna mitindo ya maisha inachangia katika tatizo la afya ya akili, hususani kwa vijana. Kwako Happiness.

Audio Credit
Anold Kayanda/Happiness Pallangyo
Audio Duration
7'50"
Photo Credit
© WHO/Ploy Phutpheng