Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNCDF/Video

Maji ni uhai na yanabadili maisha ya watu na jamii zao:UNCDF

Mradi wa nishati ya maji wa  AHEPO upo katika kijiji cha  Lifakara kwenye maporomoko ya Mbangamao kwenye mto  Mtandasi wilayani Mbinga mkoani , Ruvuma Kusini mwa Tanzania.

Mradi huo ambao unafadhiliwa na shirika la mitaji la Umoja wa Mataifa UNCDF unalenga sio tu kuwapunguzia adha wananchi wa wilaya hiyo bali pia kubadili kabisha maisha yao ya kiuchumia na kijamii kwa kuwapata nishati mbadala kwani fursa ya nishati ni kitovu cha maendeleo ya jamii yoyote na ni moja ya mambo ya lazima katika kukidhi mahitaji muhimu na ya msingi ya binadamu.

Sauti
4'56"
Picha ya UN

Afya kwa vijana balehe ni msingi mzuri wa kuyafikia malengo mengine ya maendeleo endelevu – Mulika Tanzania

Shirika la vijana nchini Tanzania linalofahamika kwa jina Mulika Tanzania, ambayo ni asasi ya kiraia yenye  lengo la kuwahimiza vijana kushiriki katika miradi  mbalimbali yenye fursa ili waweze kujikwamua kiuchumi, kisiasa na kijamii sasa limejielekeza katika kuhamasisha maisha yenye afya kwa vijana kwani bila afya, itakuwa vigumu kuyafikia malengo mengine ya maendeleo endelevu yanayohamasishwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo kuu la kuyafikia yote ifikapo mwa ka 2030. 

Sauti
4'14"
UN Photo/Tobin Jones

WFP kuongeza usaidizi katika pembe ya Afrika

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP limetangaza kuongeza usaidizi katika Pembe ya Afrika wakati huu ambapo kiwango cha njaa kinazidi kuongezeka baada ya ukame wa mfululizo, na tishio la njaa linazidi kutanda.

Tangu kuanza kwa mwaka huu, zaidi ya watu milioni tisa wameingia katika uhaba mkubwa wa chakula kote katika nchi za Ethiopia, Kenya, na Somalia, na kuwaacha watu milioni 22 wakihangaika kupata chakula cha kutosha.

Sauti
4'30"
UN News/Assumpta Massoi

Asante UNDP Tanzania sasa wanawake Kigoma tunaona matunda ya kuweko kwenye vikundi

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP limejizatiti kusaidia mipango ya kuinua wanawake na vijana kwa  kupatia makundi hayo mitaji. Hilo linafanyika mkoani Kigoma nchini Tanzania ambako uweko wa wakimbizi ulibainika kuleta changamoto katika upatikanaji wa  mahitaji siyo tu kwa wakimbizi bali pia kwa jamii za wenyeji ambao wanawapatia hifadhi.

Sauti
4'46"
FAO

Chukua hatua zifuatazo kuepusha sumu kuvu kwenye mazao

Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake ikiwemo lile la chakula na kilimo, FAO pamoja na lile la afya duniani, WHO yanapigia chepuo umuhimu wa kukabiliana na sumu kuvu kwenye mazao. Hii ni kwa kutambua kuwa sumu kuvu sio tu ina madhara kwa afya ya binadamu bali pia ni moja ya sababu kubwa ya upotevu wa mavuno ya mazao. Uhifadhi duni wa mazao kama vile mahindi, karanga husababisha mazao hayo kupata sumu kuvu na hivyo yasiweze kuuzika na pia iwapo mtu atanunua na kula basi anaweza kupata madhara ya kiafya. Je sumu kuvu ni nini?

Sauti
3'26"
UN/Anold Kayanda

TEDI Tanzania tunalenga kuhamasisha kuwe elimu inayoendana na hali ya sasa duniani

Asasi isiyo ya kiserikali ya TEDI Tanzania, katika kutekeleza Lengo namba 4 la Maendeleo Endelevu linalohusu elimu bora, imeamua kulitekeleza lengo hilo kupitia kampeni yao ya kuishawishi serikali na wadau wengine kuboresha ubora wa elimu nchini Tanzania kuanzia ngazi ya msingi hadi taasisi ya elimu ya juu kwa kuziba pengo kati ya nadharia na vitendo kupitia kuunganisha ujuzi wa vitendo ambao hautolewi katika mtaala wa kawaida wa elimu elimu. Gloria Anderson, Mkurugenzi wa shirika la TEDI Tanzania ambalo linahamasisha elimu inayoendana na hali ya sasa ya sayansi na teknolojia ili

Sauti
4'8"
MONUSCO/TANZBATT_9

Kiswahili: Juhudi binafsi za kukiendeleza sambamba na kinavyoleta ahueni kwa walioko kwenye mizozo

Zaidi ya mwezi sasa umepita tangu maadhimisho ya kwanza ya lugha ya Kiswahili duniani na harakati zinaendelea kusongesha lugha hiyo adhimu. Ni katika nyakati kama hizo watu wanaanza kutambua umuhimu wa lugha yoyote katika maendeleo na hadi kupatiwa hadhi ya kimataifa inakuwa juhudi nyingi zimefanyika. Ziko juhudi binafsi, za kikanda na za kimataifa ambazo zinawezesha lugha kutumika hata pale penye mazingira magumu ili kuleta ahueni kwa wenyeji.
Sauti
4'8"
Leah Mushi

Vijana tuaminiwe tunapoanzisha mashirika - Suzan

Tarehe 12 mwezi huu wa Agosti dunia itaadhimisha siku ya Vijana duniani chini ya kauli mbiu Mshikamano wa vizazi: Kuunda Ulimwengu kwa Vizazi vyote, lengo likiwa kuhakikisha rika zote kwenye jamii zina mshikamano na vijana wanaweza kufikia malengo ikiwa ni pamoja na kutafuta suluhu za changamoto katika jamii zinazowazunguka.

Sauti
4'1"